SWALA 490     PAL 400     TTP 120     MCB 500     JHL 5,800     YETU 550     EABL 3,320     TCCL 500     MBP 490     KA 80     TICL 350     DCB 265     KCB 770     MUCOBA 400     TBL 10,900     NICO 165     NMG 340     TCC 17,000     SWIS 1,180     TOL 550     CRDB 165     DSE 880     NMB 2,340     TPCC 2,500     VODA 770     MKCB 780     USL 5     

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

UZINDUZI WA HUDUMA YA UWEKEZAJI KUPITIA INTANETI
 

Leo Tarehe 5 Mei 2017 Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE) likishirikiana na  Kampuni ya Kitanzania Maxcom Africa – Maxmalipo,  limezindua mfumo wa mauzo na manunuzi ya hisa kwa njia ya mtandao wa intaneti.

DSE tunayo furaha kubwa sana kuzindua mfumo huu madhubuti ambao unawezesha Watanzania waliopo popote duniani kushiriki katika soko letu la hisa.

Katika uzinduzi huu Maxcom Africa ambao ni wavumbuzi wa mfumo huu wameeleza kwamba,  mtumiaji yeyote anaweza kununua hisa na kulipia kwa njia  ya Mitandao ya simu iliyopo Tanzania (Mpesa,Tigopesa,Airtel Money), kadi za benki (Visa au Master Card) na pia kupitia mawakala wa Maxmalipo popote nchini.

Bw. Deogratius Lazari ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu, Maxcom amefafanua kwamba: “mteja anaweza kununua hisa kwa kuingia kwenye Tovuti ya DSE (www.dse.co.tz) na kuchagua menyu ya “Trade Online”  au kuingia kwenye  www.trade.dse.co.tz  ili kuweza kuingia kwenye mfumo huu mpya”.

Kitendo cha mteja kuingia kitampa nafasi ya kusajili akaunti na kuchagua hisa za kampuni kwa ajili ya manunuzi na kisha kufanya malipo kwa njia zilizo ainishwa.

Katika Uzinduzi huu Bw. Patrick Mususa amefafanua kwamba: “katika mageuzi makubwa ya masoko ya hisa ya Afrika Mashariki, DSE imekua kwa kipindi kifupi sana ukifananisha na masoko mengine ya nchi jirani”. Pia Bw. Mususa amefafanua kwamba: “kwa Kipindi cha Miaka 3 Soko la hisa la Dar es Salaam limefanikiwa kuongeza Washiriki Zaidi ya Laki 2, hii ikiwa imechangiwa na kuraisishwa kwa upatikanaji na ushiriki katika soko la hisa kwa kutumia simu za kiganjani (Mobile Trading  *150*36#). Kwa kipindi chote hiki Soko la hisa limeshirikiana na kampuni za wazawa kurahisisha ufikiwaji wa soko na idadi ya ushiriki katika minada yake”.

DSE inatoa rai kwa watanzania kushiriki katika manunuzi ya hisa kwa njia hii ya mtandao ikijumuisha watanzania walio ndani na nje ya nchi (Diaspora).

Imetolewa na:

 

Menejimenti

Dar es Salaam Stock Exchange PLC