SWALA 490     MBP 490     VODA 770     TCCL 470     NMG 315     MKCB 780     CRDB 235     DCB 265     SWIS 1,120     TOL 550     MUCOBA 400     MCB 500     TTP 120     JHL 5,850     TICL 350     TCC 17,000     NMB 2,340     EABL 3,120     TBL 10,900     PAL 400     YETU 550     USL 5     KA 80     KCB 750     DSE 960     TPCC 2,500     NICO 185     JATU 1,440     

PRESS RELEASE: DSE INITIAL PUBLIC OFFERING (IPO)_KISWAHILI

TAARIFA KWA UMMA:
KUHUSIANA NA UUZWAJI WA AWALI (IPO) WA HISA 15,000,000 ZA
DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE PLC (DSE)

 

Kampuni ya Dar es Salaam Stock Exchange PLC (DSE) inatangaza rasmi uuzwaji wa awali (IPO) wa hisa Milioni 15 kwa bei ya shilingi 500/= kwa kila hisa moja.
Mauzo ya awali (IPO) yataanza Jumatatu tarehe 16 Mei 2016. Mauzo yataendelea kwa wiki 3 na kufungwa rasmi saa kumi alasiri kwenye tarehe 3 Juni 2016. Kufuatia kufungwa kwa mauzo ya awali DSE itajiorodhesha katika soko la hisa Dar es Salaam ili kuziingiza hisa hizo katika soko la pili la (yaani secondary market) ili kuwezesha wanahisa kuuza na kununua hisa zaidi kwa bei itakayoamuliwa na nguvu za soko.
Mauzo ya hisa na kujiorodhesha katika soko la hisa la Dar es Salaam inafuatia mahitaji ya kisasa ya masoko ya hisa na yamekusudiwa kuleta ubora na tija katika utendaji wa uongozi wa DSE na zaidi katika kuimarisha utekelezaji wa mikakati na utendaji wake.
Orbit Securities Company Limited ni mshauri mkuu wa hili zoezi na CRDB BANK PLC itakuwa benki husika katika mapokezi ya mitaji yote itakayopatikana.
Wawekezaji wanashauriwa kusoma waraka wa matarajio (yaani Prospectus) ili kuwasaidia kupata taarifa zaidi na hivyo kufanya maamuzi sahihi. Nakala za nyaraka za matarajio zenye taarifa kuhusu hisa zinazouzwa zinapatikana katika ofisi za DSE; tovuti ya DSE www.dse.co.tz; ofisi za madalali wa soko la hisa Dar es Salaam; na matawi mbali mbali ya benki ya CRDB.
 
Ratiba ya Matukio Muhimu  
Tukio  Tarehe
Kuanza kwa Mauzo 16 Mei 2016
Kufunga Mauzo 03 Juni 2016
Ugawaji wa Hisa 10 Juni 2016
Kutangaza Matokeo 16 Juni 2016
Kusajilisha Akaunti za CSD 24 Juni 2016
Kuratibu hundi za malipo 30 Juni 2016
Kujiorodhesha na Kuanza Mauzo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam 12 Julai 2016

  

Aina za Malipo
Malipo kwaajili ya hisa yanaweza kufanyika kwa njia zifwatazo:

  1. Matawi yote ya CRDB Bank PLC
  2. Madalali wa soko la hisa Dar es Salaam
  3. MAXMALIPO
  4. Kupitia huduma ya “Hisa Kiganjani” kwa kupiga namba *150*36# na kuchagua “Nunua Hisa za DSE” baada ya usajili.

 

Kwa taarifa zaidi, tafadhali rejea nakala ya muhtasari wa kampuni ya DSE.
Kama mwekezaji akiwa na mashaka au dukuduku ni vema awasiliane na mshauri wake wa uwekezaji, Dalali wa Soko la Hisa, Mwanasheria, Afisa wa benki, au Mshauri yeyote wa masuala ya fedha.

 
Imetolewa na:
 
Menejimenti
Dar es Salaam Stock Exchange PLC